GET /api/v0.1/hansard/entries/1085031/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1085031,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1085031/?format=api",
"text_counter": 30,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika, kwanza namshukuru ndugu yangu, Seneta wa Kaunti ya Mombasa, Sen. Faki, kwa kuleta ombi hili la wafanyikazi wa KUSCO. Wafanyikazi 171 sio wachache. Tusiangazie wafanyikazi hawa pekee yao. Wafanyikazi hao wanafamilia; mabibi, ndugu, watoto na watoto wa ndugu wanaowategemea. Familia za kiafrika, watu hutegemeana na kushirikiana sana. Mara kwa mara wafanyikazi wengi huwa wanaishi hata na watoto wa ndugu pasi na familia yake. Familia za kiafrika ni kubwa. Wafanyikazi 171 ni nambari kubwa. Mfanyikazi mmoja anaweza kuwa anategemewa na watu zaidi ya mia moja. Ni kosa kubwa kwa wafanyikazi wa KUSCO kukosa kulipwa ridhaa zao. Wizara ya Leba inayoshughulikia wafanyikazi ilichagua afisa mmoja aliyeshughulikia jambo hili la wafanyikazi kuvutwa kazi kiholela. Afisa huyo aliandaa ripoti iliyosema kwamba wafanyikazi hao walivutwa kazi kiholela. Afisa huyo alipendekeza wafanyikazi hao kulipwa na kampuni hiyo lakini kampuni hiyo ilifanya uwerevu na kuuza kampuni hiyo. Kampuni hiyo ilififia na hatimaye kufungwa. Mambo kama haya yanatendeka kila mahali katika nchi yetu. Katika Kaunti ya Kilifi, makampuni mengi yanatumia wafanyikazi na baadaye wanafunga na kuwaacha katika hali mbaya maishani. Wengi wa wafanyikazi walioachishwa kazi wana watoto shuleni. Madhara kama haya ya kuwachishwa kazi yanaleta hasara kubwa katika familia kama ndoa kuvunjika, nyumba kuvunjika, watoto kuacha shule na mengine mengi. Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba watoto wa kike huwa katika hali mbaya zaidi kwa sababu hawana la kufanya hivyo wanalazimika kufanya kazi ambazo hawangefanya kama wangesoma. Mambo kama haya yanatendeka katika kampuni kama za Export Processing Zones (EPZs). Kamati ya leba na ustawi wa jamii inayoongozwa na ndugu yangu seneta wa Nairobi, Sen. Sakaja, inafaa kukemea kitendo hicho na kufanya uchunguzi kwa kina The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}