GET /api/v0.1/hansard/entries/1085102/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1085102,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1085102/?format=api",
    "text_counter": 101,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Mimi pia ninachukua fursa hii kujiunga na Maseneta wenzangu kumpongeza Sen. Mwangi kwa kazi nzuri ambayo amefanya. Aliwahi kuzuru sehemu ya Jomvu Kuu siku moja na tukaenda mpaka Ukunda siku hiyo hiyo. Tukimaliza ziara ya shamba la Ukunda ilikuwa ni karibu saa mbili usiku. Naipongeza kamati yake kwa kazi nzuri wanayofanya. Pia ningependa kujiunga na Seneta Dullo kusema kwamba kuwe na mwelekeo wa kuonyesha hii ripoti itatekelezwa vipi kwa sababu maswala mengi ya ardhi yameweza kufa kwa NLC. Kwa hivyo, hatungependa ripoti hii, ambayo Kamati imekaa, ikafanya kazi kubwa iende kuishi katika shelves za NLC kama vile ripoti zingine zilikufa huko. Asante, Bw. Spika."
}