GET /api/v0.1/hansard/entries/1085161/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1085161,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1085161/?format=api",
"text_counter": 160,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Ninampongeza Sen. Khaniri kwa kuleta Taarifa hii. Kamati ambayo itapewa Taarifa hii iishughulikie kwa umuhimu ufaao. Taarifa yenyewe ina mambo muhimu ambayo yanasumbua vijana wetu. Ukosefu wa kazi baada ya kuja kwa hili janga la korona umekuwa kizungumkuti. Waendeshaji boda boda na wafanyibiashara wa jioni wameathirika sana kwa sababu ya curfew. Mwishowe, wanakosa ajira. Wanaowategemea ni wazee. Wazee nao ndio wanaathiriwa zaidi na ugonjwa huu wa korona. Hawa wazee wanaugua magonjwa tofauti na sasa inakuwa vigumu kununuliwa dawa. Sasa wazee wanaathirika zaidi na wanakufa kutokana na ugonjwa huu. Kamati itakayopewa fursa ya kuangalia Taarifa hii wanapasa kuishughulikia zaidi. Nimesikia kunapasa kuwa na Kamati ya muda na mimi ninaunga mkono. Watakuwa na majukumu ambayo yatalenga tu maswala ya kushughulikia ugonjwa wa korona. Inapasa kujulikana wazi kwamba umuhimu wa Serikali ni kushughulikia wananchi wake. Wakati huu wa hili janga, Serikali inapaswa kupunguza ushuru. Kwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}