GET /api/v0.1/hansard/entries/1085162/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1085162,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1085162/?format=api",
    "text_counter": 161,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "mfano, ushuru wa gesi na kadi za mawasiliano zimeenda juu. Hizi ndizo bidhaa ambazo wananchi wa kawaida wanategemea. Hata hivyo, inaonekana Serikali haina haja na wananchi wake. Wanaendelea kutoza ushuru kila mahali nao wananchi wanazidi kusononeka. Ushuru unapochukuliwa, kama vile Sen.Wetangula alivyosema, baada ya sisi kufanya mgao wa pesa kwa kaunti zetu, magavana wanashughulika kusema ya kwamba wanafanya majukumu ya kuwezesha wananchi kujua kuhusu Korona, ilhali kila mtu ambaye yuko katika sehemu ya Kenya anajua kuhusu Korona. Hakuna haja ya kusema kwamba unahamasisha wananchi kuhusu Korona. Unapaswa kutengeneza hospitali zetu ili wagonjwa wakienda kule, wapate dawa, vitanda na vifaa ambavyo vinahitajika. Nakubaliana na ndugu yangu Sen. Khaniri vile alivyoleta hiyo taarifa kwamba tunafaa tujifunge kibwebwe tupambane na hii hali na itawezekana tukitengeneza hili jopo ndogo la kuweza kuangalia hayo kwa mapana na marefu. Asante."
}