GET /api/v0.1/hansard/entries/1085167/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1085167,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1085167/?format=api",
"text_counter": 166,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante Bi Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Ningependa kumsifu ndugu yangu Sen. Khaniri kwa kuleta Hoja hii kuhusiana na mambo ya Korona. Tunaelewa ya kwamba ni karne kuanzia sasa ambapo ugonjwa huu haukuwa katika ulimwengu. Lakini karne hii imeleta maradhi aina ya Korona ambayo imeleta huzuni katika familia nyingi sana, sio katika Kenya pekee yake lakini katika ulimwengu mzima. Hatari ambayo Serikali yetu haijazingatia ni kwamba haijatia mkazo vile inaweza kuzingatia jinsi watu wa Kenya wanaweza kuishi ili waweze kuepukana na hili janga la Korona. Tumeona ya kwamba Wakenya wengi wameweza kupoteza kazi. Kazi zilikuwa zikifanywa kuanzia asubuhi mpaka jioni lakini siku hizi masaa yamepunguzwa. Hapo awali, kazi iliyokuwa inafanywa na watu 100 unapata sasa wafanyakazi wamepunguzwa wamekuwa watu 50. Tumeona shida nyingi zimetokea katika nyumba nyingi na hili sio jambo la kawaida katika maisha yetu kama Wakenya. Tumeambiwa tuvae barakoa lakini barakoa pekee yake hazitafaa kama ufisadi wa kuzingatia jinsi hizi dawa ambazo zinaletwa kama msaada wa Kenya hautatolewa. Serikali yetu inatenga pesa za kuenda katika mashinani. Tumeona kuna watu wanaitwa COVID billionaires. Zamani walikuwa maskini lakini kwa sababu ya huu ugonjwa wa Korona, watu baadala ya kusaidia wananchi wanatumia hii misaada ama kuweka pesa ambazo zimepelekwa katika serikali zetu za kaunti, kwa mifuko zao. Hili sio jambo nzuri. Serikali inafaa kutilia mkazo na kuweka mikakati maalum ili pesa zinazoplekwa mashinani zinatumika kusadia wananchi wanaopelekewa hizi pesa."
}