GET /api/v0.1/hansard/entries/1085701/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1085701,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1085701/?format=api",
"text_counter": 110,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, nimesimama kuambatana na Kanuni ya 48(1) za Kanuni a Kudumu za Bunge la Seneti ya Kenya kuomba kauli kutoka kwa Kamati ya Habari, Masailiano na Teknologia kuhusu kucheleweshwa kwa ulipaji wa mishahara ya wafanyikazi wa Shirika la Posta nchini. Katika Kauli hiyo Kamati hiyo inapaswa: i) Kueleza sababu za shirika hilo kuchelewa mara kwa mara kulipa mishahara ya wafanyikazi wake. ii) Kueleza sababu za shirika hilo kuchelewa kulipa kodi, pesa za huduma ya afya, pesa za uzeeni na mikopo ya wafanyikazi ilhali wanadaiwa na vyama vya Ushirika (SACCO) pamoja na benki za kibinafsi. iii) Kueleza hali ya kifedha ya shirika hilo ikifikiriwa kwamba wafanyikazi wake huenda wakakosa ajira iwapo shirika litafilisika."
}