GET /api/v0.1/hansard/entries/108578/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 108578,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/108578/?format=api",
    "text_counter": 676,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Machage",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Roads",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Jambo la utawala kufikia jamii zilizonyanyaswa tangu siku za awali za ukoloni mpaka sasa, namshukuru sana Bw. Kioni, hata ingawa anatoka kwa jamii kubwa, amependekeza hayo mabadiliko, kusudi sisi tuone kwamba sio jambo ambalo linasisitizwa tu na jamii ndogo; hata zile kubwa za wenzetu, ndugu na dada zetu walioko katika hili Jumba, nashukuru. Lakini hiyo shukrani itapita na upepo kama sisi wote hatutajitolea na kuonekana kwa taifa hili kwamba Kenya ni nchi ya wote. Historia itaandikwa leo kwamba jamii kubwa, hasa wale ambao wamejitokeza na kwenda nyumbani, kwamba hawajali maslahi ya wanyonge. Kwamba, wao hawatakuwa na shida kesho wakija kwetu kutafuta kura. Naomba; napiga magoti, wote ambao tuko hapa kama hata hatutoshi, tuweke sahihi kwamba, tunaona wanyonge Kenya hii."
}