GET /api/v0.1/hansard/entries/1086142/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1086142,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1086142/?format=api",
"text_counter": 46,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": " Mhe. Spika natoa kongole na kukubaliana na mwenzangu Mhe. Tandaza. Kama walivyozungumza Wajumbe kadhaa, masuala ya ardhi ni tetesi, hususan huko kwetu maeneo ya Pwani. Nataka kutoa mfano wa eneo lile natoka mimi la Mvita. Kihistoria, kuna baadhi ya watu waliopatiwa ardhi hizi sio kwa sababu nyingine lakini walipatiwa kwa niaba ya wakaazi wa Mvita na Mombasa kwa jumla. Na hii ilikuwa kabla Kenya kupata uhuru. Ardhi hizi walipatiwa watu waliokuwa wanaitwa sultan kwa sababu walikuwa na mamlaka ya maeneo yale. Wakati wa aliyekuwa Mbunge wa Mvita, marehemu Shariff Nassir, Mungu amuweke pema palipo na wema, alihakikisha Wizara ya Ardhi ilienda katika maeneo yale na Rais Mstaafu, ambaye pia ameenda mbele ya haki, Daniel arap Moi, alitoa amri ya kuwa ardhi za mbele za eneo hili watu walipe Sh30,000 na za nyuma Sh15,000 kwa sababu ya ile historia. Nakumbuka ya kuwa baadhi ya watu walilipa na baadhi wakapewa stakabadhi zao. Huu wakati wangu mimi, niliweza kuenda na National Land Commission, ambayo ni kamisheni inayotambulika kikatiba. Walitoa amri kwa zile ardhi, kwa saabu ya historia ya mahali pale, watu walipe Sh400,000 na Sh500,000 ili wapatiwe ardhi zao Mpaka sasa hivi, kuna wengine wanaona kuwa watu wazima wanaweza kutishwa"
}