GET /api/v0.1/hansard/entries/1086420/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1086420,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1086420/?format=api",
    "text_counter": 324,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii nichangie katika Mswada huu ambao umetoka Bunge la Seneti. Nataka niseme vile wenzangu wamechangia. Kuna baadhi ya vipengele katika Mswada huu na haswa kile kimegusiwa sana ni kwamba yule anatakikana kuwa mwenyekiti wa bodi hii lazima awe na shahada ya digrii. Nataka niunge mkono na kusema kwamba iwapo mwenyekiti atakuwa na shahada ya digrii, ni lazima tuhakikishe naibu wake pia ana shahada ya digrii. Ni kweli kwamba katika kaunti zetu - na mwenzangu Mhe. David Ochieng’ alikuwa ameongea - kulikuwa na baadhi ya magavana waliopendekeza kwamba tuwe na Mswada kama huu. Huenda ikawa walikuwa na malengo ya kuhakikisha kwamba kaunti zetu ziwe nzuri. Unaweza kuona kwamba katibu katika bodi hajaangaziwa na hawajasema kama atakuwa na shahada ya digrii au itakuwa namna gani kwa sababu yeye akiwa hapo kama mwandishi, lazima awe na shahada. Ni kweli mwandishi katika Bunge ambaye anasimamia masuala katika Bunge ni tofauti na mwandishi katika bodi kwa sababu mwandishi mwenye ako katika bodi anapambana na malengo katika bodi hiyo. Hata hivyo, mwandishi mwenye ako katika serikali ya kaunti ni yule anapambana na mikakati ya kaunti. Wakija kupiga kura katika kamati hiyo, unaona kwamba huyu katibu hawezi kupiga kura. Anaonekana kwamba ana mamlaka na iwapo anaenda kupewa mamlaka hayo, anatakikana awe ni mtu mwenye shahada ya digrii. Natofautiana na wengine ambao wamesema lazima iwe shahada katika taaluma ya ufanyikazi. Yeyote atakayekuwa na masomo ya digrii atahitimu kufanya kazi hiyo kwa sababu itakuwa ni kazi ya bodi. Naona mtu mwenye ako na shahada katika kitengo kingine anaweza kushikilia hii kazi na kuifanya. Kusema ukweli, tumekuwa na changamoto katika kaunti zetu. Wale waliochaguliwa kama mawaziri hawaelewi kazi yao ni ipi."
}