GET /api/v0.1/hansard/entries/1086528/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1086528,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1086528/?format=api",
"text_counter": 102,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Kupitia kwa Kanuni za Kudumu 44(2)(c), ninaomba jawabu kutoka kwenye Mwenyekiti wa Kamati ya Afya kuhusu mambo ya waendeshaji wa mabasi ya abiria wakati huu wa janga la COVID-19 katika nchi yetu. Twakubali na hatupingi kuwa reli na usafiri wa anga unabeba wateja wasafiri zikiwa zimejaa wakati huu wa janga la COVID-19. Lakini, gari za abiria, zinazofika zaidi ya elfu moja, mia mbili na sitini kupitia kampuni arobaini na mbili, zinabeba zikiwa na nusu abiria na wamekatazwa usafiri wa usiku. Kampuni kadhaa zimefungwa, watu hawajalipwa mishahara, wengine wamefutwa kazi, na hali yazidi kuwa ngumu kwao. Washika dao wakiwemo NTSA na wenye kampuni wenyewe hawakuhusishwa katika mpango wa Wizara ya Afya. La kueleweka ni kuwa, mwelekeo ama kanuni zilizowekwa sahihi na Waziri wa Uchukuzi, Barabara, Ujenzi wa Miradi ya Umma, ujenzi wa ukarabati wa barabara, reli na majengo, viwanja vya ndege, bandari na makazi, Februari 2021 hadi leo hazijatekelezwa. Kupitia haya, ningeomba jawabu kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Afya: i. Ni kipi kilichosababisha reli na anga kukubaliwa kubeba wateja ikiwa imejaa ilhali, mabasi yanabeba yakiwa nusu? ii. Wizara itafakari na kuweza kurejelea mipangilio, hamu ama uwezo wa sheria hizi zinazowaumiza Wakenya hususan wakati huu ambao ni mgumu. iii. Usafiri wa usiku ukubaliwe kama vile usafiri wa reli na anga umeweza kukubaliwa na unaendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja. iv. Ni kwa nini kanuni ziliwekua sahihi na Waziri wa Usafiri Februari 2021 hadi leo hazijaweza kufuatiliwa wala kutekelezwa?"
}