GET /api/v0.1/hansard/entries/1086953/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1086953,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1086953/?format=api",
    "text_counter": 527,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Vile vile, wakulima wetu kupata hisa hamsini na moja katika kampuni ambazo ni za watu binafsi na pia katika zile kampuni za kusaga, itawapatia nguvu sana wakulima wetu wa miwa. Hilo litakuwa ni jambo la kupunguza wale watu ambao wana ubinafsi katika mambo ya uchumi wa sukari. Vile vile, wakulima wengi hawajalipwa malipo ya fedha zao katika kilimo hiki. Hivi sasa, kupitia bodi hii ambayo itakuwa imetengezwa na sheria hii ya sukari ambayo inaitwa Sugar Act, hayo mambo yote hayatakuwa changamoto, bali litakuwa ni jambo la kuboresha mambo hayo."
}