GET /api/v0.1/hansard/entries/1087306/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1087306,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1087306/?format=api",
"text_counter": 83,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Mara nyingi, Serikali imekuwa ikitilia mkazo zaidi mambo ya hospitali. Hivi juzi, imetilia mkazo zaidi upande wa virusi vya korona. Imetilia mkazo pia upande wa cancer . Hiyo ni sawa kabisa. Lakini kwa upande mwingine, Serikali imelegeza mkono hususan kwa watu wenye akili punguani. Hapa nchini, ni hospitali chache ambazo zinatoa matibabu kwa watu wenye akili punguani. Ninavyoelewa mimi, zipo hospitali mbili tu ambazo zinajulikana sana kwa kutoa matibabu kwa wagonjwa wa aina hii. Katika sehemu ya pwani, Hospitali ya Port Reitz ndio inajulikana sana. Ukija Mji wa Nairobi, ni Mathari National Teaching and Referral Hospital. Hospitali ya Serikali iliyoko Port Reitz haina vifaa vya kutosha. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}