GET /api/v0.1/hansard/entries/1087307/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1087307,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1087307/?format=api",
    "text_counter": 84,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Jambo la kusikitisha ni kwamba hivi leo ukiambiwa kwamba mtu wako amepatikana na akili punguani na ameambiwa aende Port Reitz utashangaa ukienda pale, ukiona vile wale watu wenye akili punguani wanavyoishi. Wanawekwa katika hali dhaifu ya kwamba hata pengine kama ulikuwa umeenda pale na huna akili punguani kama vile alivyosema huyu ndugu yangu Sen. Mutula Kilonzo Jnr., sisi sote kama binadamu inafika wakati ambapo akili zetu zinapungua, basi ukifika pale utashikwa na akili punguani kwa sababu ukosefu wa vifaa na hali ya udhaifu. Bw. Spika, ninaona ya kwamba ingekuwa vizuri ikiwa Serikali itahakikisha ya kwamba kila kaunti iwe na uwezo, kama kaunt yangu ya Kilifi ambayo ya kuweza kutenga mahali ambapo hawa wagonjwa wenye akili punguani wanaweza kuangaliwa kwa hali ya heshima na kuwekwa kwenye mahali safi. Hiyo taarifa aliyosema ingekuwa vyema kama ingetiliwa mkazo na tuwezekuangalia kwamba hawa ndugu zetu ambao watakuwa wamepatikana kuwa na akili punguani waweze kuangaliwa kisawa sawa. Asante, Bw. Spika."
}