GET /api/v0.1/hansard/entries/1087312/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1087312,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1087312/?format=api",
"text_counter": 89,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika, kuna lugha ile ambayo unaweza kuitumia ikawa lugha ya fasaha. Ukisema ya kwamba yule ni mtu mwendawazimu, hiyo ni matusi kwa yule mtu ama jamii ile iliyo na yule mgonjwa mwenye akili punguani. Akili punguani ni neno ambalo limetambuliwa katika kutumia lugha ya Kiswahili kwamba mtu akiwa akili yake haiko timamu, basi anaitwa mwenye akili punguani; haitwi mwendawazimu. Kumuita mtu mwendawazimu ni kumdharau. Ni kama vile ndugu yetu yule ambaye hayupo hapa sasa Sen. Mwaura; kuna majina tofauti tunaweza kumuita. Lakini sasa tunamuita mtu mwenye ulemavu yule hawezi kujisaidia. Huwezi kumuita nguchiro, ambalo ni jina la kumdharau mtu. Kwa hivyo, ukitumia lugha fasaha ya mtu ambaye akili yake haiku sawa sawa kabisa unaweza kumuita mtu mwenye akili punguani. Ningependa kumfahamisha ndugu yangu Murkomen kwamba yuko sawa vile alivyosema na mimi naona kwa upande wangu pia niko sawa vile nilivyosema. Lakini katika lugha ya ufasaha ni kwamba hawa watu wenye akili imepungua kidogo kabisa ni akili punguani. Asante, Bw. Spika."
}