GET /api/v0.1/hansard/entries/1087314/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1087314,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1087314/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Murkomen",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 440,
"legal_name": "Onesimus Kipchumba Murkomen",
"slug": "kipchumba-murkomen"
},
"content": "kujifunza. Mara nyingi tumesema ya kwamba kama vile Bunge ya Kitaifa imefanya tayari ya kwamba ile Standing Orders yetu itafsiriwe iwe katika lugha ya Kiswahili ili wengine wetu tupate nafasi ya kujifunza kupitia hizo Standing Orders. Lakini ningependa ndugu yangu Sen. Madzayo akubaliane na mimi ya kwamba ninahisi ya kwamba akili punguani inaweza eleweka na watu huko nje kuwa kama matusi. Ni kama kumuita mtu mwendawazimu. Hata kama mimi sio mkufunzi wa Kiswahili, lugha ambayo inafaa ni kusema ya kwamba mtu ana shida ya afya ya kiakili ama ugonjwa wa kiakili. Lakini tukisema akili punguani, vile ninavyoielewa lugha ya mtaa ile tunayotumia kule nje itawezekana kwamba hakuna mtu atajitokeza kufika kwa daktari kusema “Nitibu, niko na akili punguani.” Asante, Bw. Spika."
}