GET /api/v0.1/hansard/entries/1087350/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1087350,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1087350/?format=api",
    "text_counter": 127,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "nyumbani. Wakati wakishashukishwa mahali katika kituo cha basi, wanachukua boda boda na kwenda nyumbani. Utakuja kuona kwamba boda boda ndio watu wanapewa shida zaidi sana na hivi vizuizi barabarani. Mtu amebeba abiria na anaambiwa kila safari atakayopita katika hicho kizuizi ni lazima awache Kshs50 akienda na akirudi. Utapata kwamba kama safari yake ilikuwa leo atengeneze Kshs200 atakuwa na Kshs100. Pengine ana familia ya kuangalia na ile piki piki ameikodisha na inahitaji petroli. Mwenye hiyo piki piki pia anataka kitu hapo ndani. Sasa unapata ni hasara tupu vijana ambao wanafanya kazi ya boda boda. Bi. Spika wa Muda, tunasema kwamba hivi viegezo ambavyo vinawekwa katika barabara kuzuia, nakubaliana na ndugu yangu Sen. Wetangula akisema kwamba hajaona nchi katika Afrika mzima---"
}