GET /api/v0.1/hansard/entries/1087382/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1087382,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1087382/?format=api",
"text_counter": 159,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante Bi Spika wa Muda. Mimi nikiwa kama mmoja wa wale watu ambao walikuwa Jaji na tukaweza kustaafu, ni jambo la kusikitisha sana. Tunajua koti sio jengo ama nyumba. Koti ni hakimu. Hata akiwa mahali popote, yeye bado ni hakimu. Ukimpatia Jaji hema na kiti chake cha kuketi na meza, hiyo imetosha; hiyo ni koti. Kwa watu wa Kericho ni jambo la aibu na kusikitisha kuona ya kwamba ikiwa Serikali ilkubali ama kuachilia koti kufungwa na watu wa Kericho kukaa bila mahakama, ni jambo la kusikitisha. Kuna mambo mengi sana ambayo yalikuwa yanatokea wakati nilikuwa Jaji. Nilikuwa ninapata malalamishi kwamba, vijana wadogo wamewekwa katika gereza moja pamoja na mabarobaro halafu usiku kunatokea yale mambo ambayo ndugu yetu Sen. Mutula Kilonzo Jnr. alizungumzia. Ni jambo la aibu. Tunasema kama Bunge la Seneti kuwa ni muhimu kuona ya kwamba Koti ya Kericho imerejeshwa mara moja. Hili sio jambo la kukaa kufanya mkutano. Kwa sasa haki za watu wa Kericho zimezama ndani ya maji. Kericho sio mji mdogo kama vile Kakuma. Kericho ni mji ambao uko na wafanyibiashara. Kericho ni mji ambao mambo yanaendelea, biashara na elimu. Hata uhalifu pia uko huko. Hao wahalifu hata wakipelekwa katika hizo jela, hizo jela zitazaa? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}