GET /api/v0.1/hansard/entries/1088464/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1088464,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1088464/?format=api",
"text_counter": 22,
"type": "speech",
"speaker_name": "Endebess, JP",
"speaker_title": "Mhe. (Dkt.) Robert Pukose",
"speaker": {
"id": 1458,
"legal_name": "Robert Pukose",
"slug": "robert-pukose"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Jambo hili ambapo wanyama wa pori wanavamia na kukula mimea ya wananchi ni jambo ambalo tumelizungumzia sana katika Bunge hili. Hasa, mimi nimezungumza kuhusu eneo Bunge langu la Endebess ambapo tuko na Mbuga ya Wanyama ya Mount Elgon. Jambo ambalo limeniguza katika hii Petition ni kwamba wamesema askari wanapiga wananchi. Hiyo ni ukweli kabisa. Kwa hivyo, nataka Kamati inayoongozwa na Mjumbe wa Maara, itakapochunguza hili jambo, tunataka kujua kwa nini askari wa hifadhi za wanyama pori wanashambulia wananchi. Kwa nini wanapiga wananchi? Hilo ni jambo ambalo ni nzito sana. Askari hao hata kule Endebess wamehusika katika kupiga wananchi, hata wamama ambao huenda kuokota kuni wanapigwa. Kwa hivyo, ni jambo ambalo linatakikana kushughulikiwa. Tunataka kujua ni hatua gani Wizara itachukua kwa wale askari wanaopiga wananchi. Sijui kama hiyo pia ni kati ya kazi za kuchunga wanyama ama namna gani. Kamati itakapokaa, tungependa sisi ambao tunaishi karibu na hifadhi za wanyama watuite. Ahsante, Mhe. Spika."
}