GET /api/v0.1/hansard/entries/108855/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 108855,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/108855/?format=api",
"text_counter": 953,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister of State for Special Programmes",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Bw. Spika, asante sana kwa kunipatia fursa hii na mimi pia niweze kujumuika na wenzangu katika swala hili ambalo limetutatiza hapa kwa muda wa siku 30. Miaka 47 baada ya Uhuru, tunasikitika ya kwamba Wakenya bado hatujakubaliana kuwa sisi ni watu wamoja na wanyonge wanaonekana kuwa hawana haki. Bunge hili lingekuwa limefanya uamuzi kuwa hata wale ambao ni wanyonge; wale ambao ni makabila ambayo hayana nguvu, pia wangeweza kuhusishwa ili tukiwa na Senate, iwe pia inawabeba hao waweze kusikika sauti zao za unyonge. Leo ni siku ya masikitiko kwa muda wa siku mbili tumefanya sarakasi; tumekuwa wanasarakasi badala ya kuwa Bunge la kuheshimika. Baada ya hapo, bado tunarudi kwa wananchi tukiwadanganya na kuwaambia maneno ya uongo ambayo si ya kweli. Hatuna huruma na Wakenya. Na huo ndio ukweli uliopo, kwa hivyo ninasikitika sana."
}