GET /api/v0.1/hansard/entries/1089603/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1089603,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1089603/?format=api",
"text_counter": 188,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kwa hivyo, kuwepo kwa mchapishaji katika serikali za kaunti utasaidia pakubwa msongamano wa Miswada na notisi katika ofisi ya mchapishaji mkuu wa Serikali. Vile vile, itazipa fursa serikali za kaunti kuwasilisha Miswada yake kwa wakati katika bunge za kaunti na wananchi kujua ni arifa gani zimetolewa kuhusiana na malipo na nyingine muhimu katika maisha yao. Bw. Spika, uwepo wa mchapishaji wa kaunti utasaidia kuelimisha umma katika kaunti zetu. Kupata gazeti ya Serikali rasmi Mombasa inachukuwa wiki moja kutoka Nairobi. Lakini ikichapishwa pale, itapatikana kwa haraka na wananchi watajua ni Mswada au sheria gani zimechapishwa ili wachangie wakati wa mikutano wahusika. Hii itasaidia kuchapisha Miswada kwa lugha ya Kiswahili au za wenyeji. Kwa mfano, Miswada mingi ambayo inachapishwa na mchapishaji mkuu was Serikali inatumia lugha ya Kingereza wakati wengi hawaielewi na hawawezi kuchangia kikamilifu yanayozungumziwa katika Miswada inayopelekwa katika bunge za kaunti. Kwa hivyo, mchapishaji wa serikali za kaunti, atatoa fursa Miswada ichapiswhe kwa lugha za kienyeji au Kiswahili katika maeneo yale ili wananchi waweze kuelewa yanayozungumziwa. Bw. Spika, nimeona kuna fursa ya Kenya National Law Reporting Council kuwa na rejista ya Miswada ambayo imechapishwa na bunge za kuanti. Hili ni jambo nzuri kwa sababu atakayetaka kuangalia Miswada hii itakuwa rahisi kupata kupitia kwa taasisi ya Kiserikali ambayo ina uwezo na taratibu ya kuweka rekodi. Ninaunga mkono Mswada huu ambao utasaidia pakubwa kuboresha huduma za serikali za kaunti zetu katika jamhuri ya Kenya."
}