GET /api/v0.1/hansard/entries/1089607/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1089607,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1089607/?format=api",
    "text_counter": 192,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Zawadi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Mswada huu. Yangu yatakuwa machache kwa sababu mengi yamezungumzwa. Kuna Miswada ambayo iko katika serikali za kaunti ambayo haijaona mwanga wa jua kwa sababu ya msongamano wa Miswada mingi. Lakini, kuna Mswada mmoja kule Kilifi ambao utakuwa na shida kuchapishwa. Kwa mfano, muguka unapendwa sana kule Kilifi lakini kuna Mswada ambao utachapishwa kusema kwamba watakaoleta Muguka wabandikwe magunia ya nazi wapeleka wanapotoka ili pia sisi tufaidike kutokana na bidhaa zinazotoka kaunti zingine. Pili, kuna wale ambao wanaoana kuwa District Commissioner (DC) na kuna muda unaopeanwa ili waweze kuoana. Mara nyingi, muda ule huwachwa ili ndoa ichapishwe halafu baadaye watu wanaruhisiwa kuoana. Uchapishaji huchukua muda na wengine huamua kuoana na baadaye inajulikana mmoja wao ameoa au ako na familia ingine. Hii inaweza kuepukwa kama uchapishaji ungetoka wakati unaofaa ili watu wajipange kifamilia. Kama vile wenzangu walivyochangia, ninaunga mkono kwamba kazi zita ongezeka kwa sababu kuna wasomi wengi wenye vipaji lakini hawana kazi. Kwa hivyo, nina amini itaongeza kazi na Miswada yetu itapita haraka. Serikali za kaunti pia zitakuwa na Miswada mingi ya kisheria ambayo itasaidia wananchi wetu. Vile vile, tutapeleka huduma mashinani. Hiyo ndio maana ya ugatuzi."
}