GET /api/v0.1/hansard/entries/1089845/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1089845,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1089845/?format=api",
"text_counter": 58,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bi. Naibu Spika, kwanza namshukuru dada yangu, Sen. Dullo, kwa kuuliza swali hili. Uzito wangu ni kwamba mimi ni mmoja wa Kamati ya Leba. Lakini uzito ambao unanifanya niongee ni kwa sababu ninaangalia ripoti hii ya mama mlemavu ambaye tangu azaliwe, hajakuwa sawa na wamama wengine ambao wanaweza kujitafutia lakini alipata kibarua mahali kama hapa. Tegemeo lake kubwa lilikuwa kumuona Sen. Dullo ili amweleze masaibu yaliyomkumba ili apate msaada na yamefika hapa. Bi. Spika, tunataka wafanyikazi walemavu waendelee kupata kazi. Jambo la kusikitisha ni kwamba wamefanya kazi miaka mingi pale ndani zaidi ya miaka kumi lakini leo wameambiwa waende nyumbani. Wataenda wapi? Jambo la pili, Kamati ambayo mimi ni mmoja wao ilipitisha ya kwamba waliachishwa kazi kinyume cha sheria. Kwa hivyo, hatua itakayofuata ni Kamati iseme warejeshwe kazini. Jambo la kushangaza ni kwamba Kamati inaosha mikono kama koti ya Bibilia ya Pontius Pilate aliposema ‘huyu mtu hana dhambi, lakini sasa mimi sitaki kusema nyinyi ndio mnasema’. Tunawarejesha tena kwa watu ambao walitaka kuwaadhibu. Sasa, tegemeo lao kubwa ni kwamba hapa ndio watakaopata msaada. Lakini, sisi tunawarejesha tena kwa mdomo wa simba. Kweli hao watu watapata haki kule? Mimi ninaona waamuzi huo----"
}