GET /api/v0.1/hansard/entries/1089856/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1089856,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1089856/?format=api",
    "text_counter": 69,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Nimasikitiko kwamba umempa Sen. Kinyua nafasi ya kuongea juu ya hoja ya nidhamu, lakini katika hoja yake, hakuna nidhamu yoyote ambayo imevunjwa. Bi. Naibu Spika, mapendekezo ya Kamati hayaridhishi. Wamekubali kwamba watu walifutwa kazi kinyume cha sheria. Tukiangali Kifungu cha 37 cha Sheria ya Uajiri, mfanyikazi akifutwa kiholela, anafaa kulipwa ridhaa na kama inawezekana arejeshwe kazini. Hawa wamezungushwa mwaka mzima na sasa wameambiwa wapeleke malalamiko yao kwa Wizara yachunguzwe tena. Sisi kama Bunge la Seneti, hatukubali mapendekezo hayo kwa sababu yatailetea kejeli Bunge hili. Kwa hivyo, naomba kama waliotangulia walivyosema kwamba, hii ripoti irudishwe tena kwa Kamati na waweze kutekeleza inavyopaswa kisheria."
}