GET /api/v0.1/hansard/entries/1090311/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1090311,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1090311/?format=api",
    "text_counter": 524,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bi. Naibu Spika, ninaona kuwa unamjibu na kumweleza ndugu yangu, Sen. Sakaja, sawa sawa. Wakati nilipokuwa ninazungumza juu ya wafugaji, niliongea kwa heshima. Lakini kwa sababu ulikuwa unakata kuninyamazisha, ulisimama. Sasa ninaona umejibizana na Sen. Sakaja vizuri hadi mumeelewana ilhali hukukubali kuelewana na mimi nilipokuwa ninazungumza juu ya wafugaji wa mifugo, na wafugaji wa mifugo wanaojulikana Kenya nzima ni Wamaasai--- Bi. Naibu Spika, hii ni kwa heshima. Nilipotaja hivyo, ulisimama. Nilikuhisi nikakuambia kama nilikukosea kutaja hili jina la “Maasai,” basi uketi ili niweze kuendelea. Nilisema nitatumia jina “mfugaji”. Hivyo ingekuwa vizuri, kwa maana tungekuwa tumeelewana. Sasa wewe uliposimama ulifanya mimi niketi."
}