GET /api/v0.1/hansard/entries/1091202/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1091202,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091202/?format=api",
"text_counter": 150,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada ambao umeletwa Bungeni na Sen. (Dr.) Zani. Kwanza, ninampongeza dada yangu, Sen. (Dr.) Zani kwa kuwa mahiri na kufanya kazi ya kuonekana. Tuliingia Chuo Kikuu Cha Nairobi mwaka moja naye. Yeye alipata shahada ya sociolojia na mimi ya sheria. Kwa hivyo, ninampongeza kama mwanafunzi mwenza na kumtakia kila heri katika kazi zake za useneta. Mswada huu wa ugamvi wa rasilimali ya faida ni muhimu katika nchi yetu ya kenya. Hii ni kwa sababu mali asili imetapakaa nchi nzima. Kwa hivyo, Mswada huu utasaidia pakubwa kuhakikisha kwamba jamii zinazoishi maeneo ambayo kuna mali asili zinapata kitu kuwasaidia kuboresha maisha yao. Wenzangu waliotangulia kuzungumza wametaja mbuga za wanyama pori na madini mbalimbali kama vile mafuta eneo la Turkana, dhahabu eneo la Kakamega na kwingineko, mawe meusi Kitui na madini tofauti tofauti kama yanayopatikana Kaunti ya Taita Taveta. Katika sehemu hizi zote, hakujakuwa na njia yeyote ya kuhakikisha wenyenji watapata mzuku kutokana na mali haya. Sehemu nyingi ambazo mali hizi zinapatikana kumetokea umaskini mkubwa. Watu wengi ulalamika kila mara kuhakikisha kwamba kuna usawa baina ya mwekezaji na wale ambao wanaohusika na madini yale. Kule kwetu Mombasa, madini makubwa tukonayo ni bahari. Inasikitisha kwamba hakuna chochote ambacho kinatoka bandarini ya Kilindini. Zamani, bandari ilipoanza kujengwa, jamii za Changamwe na Likoni walikuwa wanapewa loyalties kila mwaka kutokana na matumizi ya bandari. Lakini, baada ya uhuru, mambo hayo yote yaliisha. Uwanja wa Ndege wa Moi ulipojengwa, jamii husika zililipwa loyalties mara kwa mara kwa matumizi ya ardhi kwa kujengwa uwanja wa ndege. Lakini hayo yote yaliondoka wakati tulipata uhuru mwaka wa 1963. Ninavyo zungumza, imekuwa dhiki kwa watoto wetu kupata ajira Moi International Airport au Bandari ya Mombasa kwa sababu nafasi zinatangazwa kitaifa na sisi kama wenyeji hatupati aslimia tunayotakikana kupata kulingana na sheria iliyopitishwa na Bunge. Kwa hivyo, Mswada huu utasaidia pakubwa kuondoa malalamiko ambayo iko katika kila jamii inayo husiana na matumizi ya madini. Mwaka jana, kulitolewa judgement ya watu wa Bagladesh ambapo kulikuwa na kiwanda cha kutengeneza b attery ambapo waliadhirika na madini ya lead ambayo ilitoka kwenye kiwanda hicho. Watu wengi wamepoteza maisha na wengine kuumia hali ambayo imewafanya kutofanya kazi zao kama kawaida. Kwa hivyo, viwanda vinavyoanzishwa vinasaidia pakubwa kudhulumu haki ambazo wananchi wangepata kama sheria ingefuatwa. Kwa mfano, viwanda vya simiti,vinatumia madini ya Clinker ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu. Katika eneo la Mikindani, maswala ya Clinker yameibuka na nyumba nyingi katika mtaa wa Owino-uhuru katika eneo la Jomvu Kuu sub-county wameadhirika. Lakini wawekezaji hawatoi chochote kwa watu."
}