GET /api/v0.1/hansard/entries/1091206/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1091206,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091206/?format=api",
"text_counter": 154,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "ya fidia itakayolipwa kwa jamii husika. Hili ni jambo nzuri. Mambo ya faini yamezungumziwa. Ninakubaliana na Seneta wa Kericho kwa kusema kwamba faini ya million mbili ni kidogo sana. Inafaa iwe asilimia fulani ya kiwango cha pesa zinazopatikana na mwekezaji. Kila alichotoa katika eneo lile kiwe ni aslimia fulani ambayo atalipa kama faini iwapo hataweza kutimiza sheria hii. Itajulikana kwamba mtu akikosa, lazima alipe kiwango fulani ili sheria ifuatwe. Iwapo faini hii aitabadilishwa, basi kuwe na kipengeo cha kusema kwamba, mbali na kulipa faini ya million mbili, tano au kumi, lazima alipa faida kwa jamii husika. Bila ya kuzungumza mengi, ninaunga mkono Mswada huu. Tunaomba Bunge la Seneti likipitisha, ndugu zetu wa Bunge la Kitaifa waipitisha kwa sababu hii ni njia moja ya kuleta maendeleo katika jamii zetu. Asante kwa kunipa fursa hii."
}