GET /api/v0.1/hansard/entries/1091424/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1091424,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091424/?format=api",
"text_counter": 125,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Kwanza kabisa, natoa shukrani zangu za dhati kwa Mhe. Aden Duale ambaye wakati alikuwa Kiongozi wa Walio Wengi alileta sheria hii. Pia, natoa shukrani kwa kiongozi Mhe. Wangwe kwa sababu amesoma Mswada huu wa Waqf. Mswada huu umeletwa ili kuvuta ile sheria iliyokuwa inasimamia mambo ya Waqf katika taifa letu la Kenya. Sheria iliyokuwa mwanzo imeacha mikakati mingi sana ya kuongoza na kutumika kwa Waqf ama rasilimali ambazo zinasaidia katika jambo kama hili."
}