GET /api/v0.1/hansard/entries/1091425/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1091425,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091425/?format=api",
    "text_counter": 126,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Waqf ni rasilimali ama mali ambayo mtu, watu ama mashirika, wanatoa kukidhia mali hayo kwa haja ya dini ya Islam. Waqf huwa katika mikakati ya sheria za mirathi na sheria za sakada kwa mujibu wa dini ya Islam. Mara nyingi, kumekuwa na shida nyingi sana katika rasilimali ambazo zimetolewa kwa Waqf. Kule kwetu Mombasa, kuna majengo yaliyotolewa na watu kwa nia ya kusaidia katika misingi ya dini ya Islam. Kama alivyosema Mhe. Duale, pengine mtu anaweza sema kuwa kodi inayotoka kwa nyumba yake isaidie makadhi ama isaidie kulipa maustadi ambao wanafundisha madrasa tofauti tofauti katika sehemu fulani. Kuna watu wanatumia rasilimali kama hizo kama mali yao na kusahau haswa kuwa mali hizo zilitolewa kwa sababu gani. Pia, wanaacha kufuata sababu za kidini katika mali kama hayo. Vile vile, imekuwa ni shida kwa sababu watu wengine wamechukulia Waqf kama mali yao, ama mali ya jamii fulani ama mali ya watu fulani. Wasimamizi wamekuwa tangu mwanzo wanaonekana kutoka katika sehemu fulani katika taifa letu la Kenya. Lakini sasa ni wakati mwafaka wa kutengenesa kamati ya usimamizi itakayo simamia Waqf itakayohusisha makundi yanayosimamia Waislamu. Makundi haya ni lazima yawe yanajulikana isiwe kundi mtu amelitengeza kuwa la Kislam lakini kumbe lina maadhili na sababu nyingine paso sababu za kidini."
}