GET /api/v0.1/hansard/entries/1091426/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1091426,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091426/?format=api",
"text_counter": 127,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Tume ya Waqf itasaidia haswa kuleta ukweli ama accountability and transparency, vipi fedha ama mali kama ardhi na majengo ambayo yametolewa kwa Waqf yako, hali yaliyotelewa ama yanatoa mazao kiasi gani na kama mazao hayo yanasaidia jambo lilinuiliwa katika waqf. Kwa mfano, kule Mombasa, unapata nyumba ambayo imetolewa kwa Waqf lakini imekodishwa kufanya biashara ambayo ni kinyume na dini ya Kiislamu. Jengo moja kule Mombasa lilikodishwa kuweka kilabu kinachoitwa Salambo. Katika kilabu, kuna mambo ya pombe lakini katika dini ya Kiislamu, pombe ni haramu. Kwa hivyo, ni lazima kuwa jambo ambalo litanuiliwa ama biashara ambayo imetolewa kwa Waqf iwe katika misingi ya kidini na sio kinyume na misingi hiyo. Kwa hivyo, tukiwa na hii Wakf Commission, sheria hizi zote zitakuwa sambamba na zitahakikisha kwamba hakutakuwa na dhuluma dhidi ya wale ambao wamewekewa jambo kama hili liweze kuwasaidia. Kuna rasilimali ambazo zimetolewa Waqf kusaidia madrasa kadhaa, watoto mayatima, akina mama wajane na misikiti ya kidini. Lakini unapata kwamba badala ya wale wasimamizi kufanya mambo hayo ya kidini, wanachukua zile pesa kama zao ama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}