GET /api/v0.1/hansard/entries/1091427/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1091427,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091427/?format=api",
    "text_counter": 128,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "wanazipeleka katika mambo ambayo hayakunuiliwa katika zile rasilimali zilizotolewa kwa Waqf. Wakati tunachagua wale trustees ama tunateua wale makamishna, ni lazima wawe ni watu ambao watawakilisha Waislamu. Waislamu wako katika pembe nyingi sana za taifa letu la Kenya. Hiyo pia itawakilisha makundi ama organisations ambazo zinatambulika kuwakilisha Waislamu ili ziweze kufuata misingi ya kidini pasi na kufuata misingi ambayo ni tofauti. Kwa muda mrefu, watu wamekuwa hawajui hesabu wala mapato ya rasilimali ama mali kama hizi ambazo zimetolewa kwa ajili ya Waqf. Sheria hii itaweka wazi na bayana kwamba katika rasilimali ama mali haya, mapato na mazao yake ni haya. Matumizi yake yatakuwa kwa ajili ya yale matumizi yaliyonuiliwa. Pia, wakati mtu ametoa rasilimali au mali kwa mashirika ama kwa watu kadhaa katika Waqf, hawezi kurudi kusema kwamba anataka kuchukua mali yake. Ama pengine yule aliyetoa amefariki halafu watoto wake wanarudi kusema: “Hii ilikuwa nyumba ama ardhi ya baba yetu, kwa hivyo, tunataka ardhi hii.” Ukishatoa rasilimali yoyote kwa Waqf, iwe yule baba ama yeyote ambaye ametoa rasilimali kama hiyo yuko ama amefariki, hiyo rasilimali itabakia kwa ile nia aliyoinuilia yule aliyetoa Waqf. Kwa hivyo, sheria kama hii itapunguza mambo kama hayo ambayo tumeona yakileta shida sana. Kuna wakati hata unaona watu wanasukumana kwamba mali fulani haikutolewa kwa Waqf na mwingine anasema kuwa mwenyewe aliitoa kwa Waqf kwa muda fulani ama ilikuwa vinginevyo. Lazima ijulikane kabisa ya kwamba rasilimali hii imetolewa kwa Waqf kwa maisha yote, kama yule aliyeitoa yuko ama hayuko. Lazima wasimamizi wafuatilie lile lengo na madhumuni kulingana na mujibu wa kidini ya Kiislamu. Jambo kama hili halikuanza leo. Mhe. Duale amesema kwamba lilianza kitambo sana. Ni jambo ambalo linaambatana na dini yetu ya Kiislamu katika sheria za mirathi na sadaka. Ni kama tunazungumzia sadaka ya kuendelea. Kwa lugha ya Kiarabu tunasema, Sadaqatul Jariyah. Ni jambo ambalo litaendelea mpaka mwisho wa ulimwengu ama dunia. Kwa hivyo, sheria hii ni muhimu sana na itasaidia watu maskini, wajane na watoto mayatima ambao wameweka malengo haya ya Waqf. Waqf inatolewa sana sana kwa njia kama hizo ili waweze kufanikisha malengo yao ambayo yamenuiliwa katika rasilimali kama hizo. Pia, kuna watu wengi ambao wangependa sana kutoa Waqf lakini kwa sababu hapakuwa na sheria madhubuti ya kusimamia rasilimali kama hizo, huwa wanaogopa na pengine wanafanya mambo yao kibinafsi kwa sababu wanahofia pengine mambo hayatakuwa sawa. Lakini tutakapoipitisha sheria hii, kila mmoja atakuwa na ile ari ama nia ya kutoa fedha, ardhi, majengo ama njia yoyote ile anaona inaweza kuwa sadaka ya kusaidia katika misingi na mambo ya kidini. Najua kwa sasa, Wabunge wenzangu wamefahamu tume ya Waqf ni nini. Naomba waweze kuichangia na kutuunga mkono ili kuwe na mfumo na muundo msingi wa kueleweka wa kusimamia rasilimali ama mali hizi ambazo Waislamu wametoa kwa minajili ya mambo ya kidini ya Kiislamu na ibada. Naunga mkono. Asante sana."
}