GET /api/v0.1/hansard/entries/1091476/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1091476,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091476/?format=api",
"text_counter": 177,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu, CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi name nichangie. Nimejaribu kuweka alama ya nidhamu kwa muda mrefu lakini sikupata. Nafikiri katika mazungumzo haya nitamjibu Mheshimiwa. Mwanzo, ninawapongeza viongozi wa Bunge hili kwa kuweza kuleta huu Mswada. Pili, ninapongeza Tume ya Waqf iliyo chaguliwa na Rais wetu mpendwa ikiongozwa na Mwenyekiti wao, Mhe. Zuber Noor, Sheikh Juma Ngao na Gibsham Sang, Hussein Sharriff na wakili Mwanakitili. Hawa ni wasomi wenye sifa nzuri kwa jamii. Kwa hivyo, walifanya huu Mswada ukawa mzuri na tunauamini."
}