GET /api/v0.1/hansard/entries/1091477/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1091477,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091477/?format=api",
"text_counter": 178,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu, CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Uzuri wa Mswada huu sio kwamba hii sheria inatungwa sasa hivi. Ilikuwepo lakini kwa upande mmoja, tusema wa Pwani, lakini hii sheria sasa itakuwa ni ya Kenya mzima. Hapo inastahili tuelewe kwa wale ambao bado hawajaelewa. Sheria ipo lakini hii inaongeza maeneo. Pili, mambo ya pesa yameangaziwa vizuri. Itakuwa watu hawana wasiwasi kwamba pesa zimetumiwa vibaya. Mambo haya yameangaziwa vizuri katika hii sheria. Wakati wa kuomba nafasi katika tume, itakuwa mtu anatuma maombi na haitakuwa ni watu wale wale ambao watakuwa katika tume siku zote. Pia, imepatiwa nafasi na uwezo wa kujiendeleza. Kwa hivyo, ni sheria ambayo imeongezwa ili ifanye kazi vizuri. Mimi nashangaa na Mheshimiwa mwenzangu kusimama na kusudi ya kuleta taharuki hapa. Nimeshangaa haya mambo ya radicalisation yameingia vipi hapa. Hii ni kusudi tu kwa sababu wanataka ionekane kama kuna taharuki na hakuna. Mwanzo, hii sheria ikipita ndio pesa zitajulikana zinatumika na kuingia vipi na kuenda wapi kwa sababu hesabu itakuwa sawa sawa."
}