GET /api/v0.1/hansard/entries/1091478/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1091478,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091478/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu, CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Pili, si sawa kwa Mbunge mwenzetu kufanya kama lugha ya Kiswahili ni dhaifu ambayo haifai na mtu akizungumza Kiingereza ndio anakuwa msomi. Huko kwetu pwani kuna beachboys tele na wanazungumza fluent English na hawakuenda hata darasa la kwanza. Kwa hivyo, asijifanye na kizungu chake pengine amesoma na hana hekma. Waqf ni nzuri na naomba Wabunge wenzangu tushikane na kuipitisha isiwe kama kuna vuguvugu inaendelea. Kwenye mitandao tunaona wanasema Wakristo wanafanyiwa hivi na Waisalamu hawatafanyiwa hivyo. Hayo si mambo mazuri ya kuchochea hapa Kenya. Hapa Kenya tumekaa vizuri na kwa mambo ya dini tumeshikana. Kwa hivyo, tuendelee kushikana kabila na dini zote hapa Kenya."
}