GET /api/v0.1/hansard/entries/1091498/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1091498,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091498/?format=api",
"text_counter": 199,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "mwema, na tunaomba Mwenyezi Mungu kuwa tujaliwe kwa sababu ya wazee wetu kufika pema palipo na wema. Nimesikia wengi wakizungumza hapa kwamba jambo la waqf si jambo geni katika Kenya. Sheria hii imekuwepo tangu mwaka wa 1948. Tunalofanya sasa hivi ni kujaribu kuirekebisha sheria hii. Kama wenzangu wamezungumza, madhumuni ya kuifanya sheria ni iweze kuandamana pamoja na Katiba ya Kenya. Nataka tufahamu kuwa vile sheria ilivyo sasa, haya ni mapendekezo ya kuibadilisha ambayo inaweza kuhukumu masuala ya waqf. Wakiwemo ndani yake kwanza, zamani tulikuwa na Provincial Commissioners ambao katika sheria ilivyo hivi sasa ni PCs . Pili, Kadhi Mkuu wa Kenya ambaye hana kura. Tatu, Muislamu yeyote ambaye anachaguliwa na Waziri ambaye anafahamika katika sheria ilivyo, na Waziri ambaye alikua anahusika na masuala ya sheria wakati huo. Kisha, Waislamu watano ambao wanachaguliwa na gavana, sio magavana walio sasa hivi katika Katiba. Kwa wale wanaofahamu historia ya Kenya, sehemu za Pwani zilikuwa na magavana. Sheria ya mwaka 1948 inasema kuwa PC wa wakati huo angechagua kisha gavana apitishe watu watano wengine. Kuna tofauti kati ya sheria ya hapo awali na sheria ya sasa. Sasa hivi tunazungumzia watakaochaguliwa. Kwanza, ni mtu ambaye amesoma dini, pili, mwakilishi ambaye anaweza toa. Tukizungumza kuhusu wasimamizi (trustees), ni wale ambao waliotoa. Tatu, mwakilishi ambaye atakayefaidi, nne, mfanyibiashara maarufu, tano, aliyesoma sheria, wakili. Sita, mweka hesabu, mtu ambaye amebobea katika hesabu. Saba, aliyebobea katika hesabu za masuala ya ardhi, nane, anayefanya kazi na jamii, social worker. Ikiwa kuna sheria ambayo hailingani na Katiba, ni hii ambayo inafanywa sasa ama ile inazungumza kuhusu PC na magavana ndio wenye kuchagua. Tena sio kuchagua mtu yeyote, kama dada yangu alivyozungumza kuwa ni lazima mtu atakaye chaguliwa awe na nidhamu fulani. Tena wanaochaguliwa hapa, sheria hii inasisitiza kuwa ni lazima waweze kupita mtihani ulioko katika Katiba, wawe ni watu wa kisawasawa katika jamii."
}