GET /api/v0.1/hansard/entries/1091499/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1091499,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091499/?format=api",
    "text_counter": 200,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Nawaomba, nawarai na nawanasii wenzangu wote, tuangalie sheria hii kwa mtazamo wa kuweka sheria itabadili sheria iliyowekwa mwaka 1948. Sheria hii ambayo haijabadilishwa inazungumza kuwa waziri anayehusika siku atainuka na kuamua ndio siku ambayo mkaguzi ataangalia hesabu. Haimanishi kuwa hesabu zinaangaliwa. Sasa hivi watu wana vilio kuwa ardhi watu walizotoa hawajui vile fedha zimetumika kwa sababu hakuna sheria ilioko. Sheria ya sasa ambayo tunataka kuipitisha inasema kuwa kuangalia fedha zilioko ni lazima zipitie Public FinanceManagement Act and the Public Audit Act, sheria ambazo ukiangalia undani wake, hakuna anayeweza toa chake kitumike kwa ufisadi na hakuna anayeweza toa chake kitumike kwa ugaidi. Nasisitiza kuwa masuala ya waqf ni lazima yatumike. Yule anayetoa ardhi, yake isitumike kwa jambo haliambatani na dini ya Uislamu. Uisilamu haukubali ugaidi na haukubuli fedha kuchukuliwa kwa madawa za kulevya. Uislamu pia haukubali fedha zichukuliwe kwa mabaa. Sasa kuna lipi zaidi ambalo halipo, halijangaaliwa, halijazingatiwa, halijawekwa katika nyoyo zetu ili tuangalie haya? Tena nasisitiza tuangalie Chuo Kikuu cha Azhar kilioko Misri. Kilianzishwa na waqf. Leo Azhar University ina zaidi ya miaka elfu moja. Waliopitia Azhar University, wamo Waislamu na wale sio Waislamu. Katika watu waliotoa ardhi zao ziwe waqf katika karne zilizopita mpaka leo, zile dhawabu na yale mazuri hayaendi tu kwa wale miili yao iko chini ya ardhi lakini nyoyo zao ziko juu, lakini kwa wale walioko sasa hivi. Ni madaktari wangapi katika dunia hii ambao wamesomeshwa kupitia waqf ? Kuna wangapi ambao wamesomeshwa na waqf? Kuna ubaya gani kesho na miaka inayokuja azuke mtoto mmoja kutoka sehemu za Western, azuke mtoto mmoja kutoka Nyanza, azuke mtoto mmoja kutoka Pwani ainuke na awe katika Bunge aseme kuwa lau isiingekuwa waqf iliyowekwa ikatumika kwa mjibu wa kisheria hangesimama hapa? The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}