GET /api/v0.1/hansard/entries/1091502/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1091502,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091502/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Mhe. Spika wa Muda, maneno yako ni kuntu. Mhe. Naibu Spika wa Muda, nilitunga sheria hii kwa sababu tulikuwa tumeona yaliyoko kuwa hakuna hesabu zinazowekwa katika mambo ya waqf. Tuliona yale yaliyoko. Ni mikakati gani zitatumika kuchagua makamishna? Nilipoleta sheria hiyo, Serikali, kupitia kwa aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi katika Bunge, Mhe. Aden Duale, aliniambia kuwa kuna sheria nyingine tayari inajadiliwa, kwa hivyo, ili tusishindane, nikubali yangu iwe nyuma. Nakubaliana na vinara wote walioko katika Bunge na nafurahi. Hata juzi tulikuwa Mombasa tukihudhuria sherehe fulani ya Idd pamoja na Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi na akaahidi atahakikisha kuwa hii sheria imepewa kipaumbele na ninashukuru. Kwa hivyo, nawasihi wenzangu waangalie hii sheria ili vizazi vijavyo viweze kufaidika kutokana na yale vizazi vilivyopita vilijaribu kufanya."
}