GET /api/v0.1/hansard/entries/1091520/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1091520,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091520/?format=api",
"text_counter": 221,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kupata fursa hii kuchangia Mswada huu wa waqf. Wengi wamezungumzia suala hili la waqf . Ningependa kueleza kwamba ni vyema kwanza tufahamu maana ya waqf ndiposa tupate yale maelezo kamili, ingawaje Mhe. Duale ametueleza. Waqf imekuweko katika nchi hii na imekuwa ikitambulika na nchi hii. Ni muongozo umekuwa ukitembea ama ukiendelezwa na Waislamu. Hivi sasa Mswada huu umefika hapa bungeni kwa marekebisho zaidi. Hii ni dalili kuonyesha kwamba umechukua mkondo wa sheria ya nchi hii inavyotakikana. Lakini, ni vyema vilevile tufahamu ya kwamba utaratibu na muongozo ambao unatakikana hususan katika suala hili, tukiwa kama Waislamu na Wakenya, unafahamu kwamba Uislamu una muongozo wake na nchi ina muongozo wake katika masuala ya dini. Ndiposa hata katika Katiba imeelezwa waziwazi kwamba kuna uhuru wa kuabudu katika dini. Kwa hivyo, nashukuru pakubwa kwamba nchi hii imetambua dini zote na miongozo yao inavyoendeshwa katika dini hizi. Hapo awali kumekuwa na waqf . Lakini kwa masikitiko makubwa, muongozo wa waqf umekuwa ukiendeshwa kwa namna ambayo hairidhishi ama hairidhishi Waislamu. Ndiposa utaratibu huu umeletwa hapa bungeni kupitia sheria kikamilifu. Tunaamini kwamba ni utaratibu ambao utakuwa na muelekeo ama muongozo kamilifu. Hili ni jambo muhimu sana katika jamii. Mara nyingi tunaona watu wanakuwa na matatizo katika elimu; watu wanakuwa na matatizo katika afya; watu wanakuwa na matatizo katika jamii. Lakini, ikiwa jamii haina muongozo katika kusaidiana katika haya, ndipo utapata kwamba huyu yuko huku anatafuta msaada na yule yuko kule anatafuta msaada. Ninaamini pakubwa malengo ya huu Mswada wa waqf ni ili wale wameelezwa kuwa na mali ya kutosha au wako na rasilimali za kutosha, wanatoa rasilimali hizi kupitia kwa kamisheni hii. Rasilimali hizi zinaweza kusaidia kuendeleza jamii kwa masuala ya elimu, masuala ya ugonjwa, na masuala mengineo ya kijamii. Ni matatizo ambayo tuko nayo. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninafikiri unayaona katika jamii. Si vizuri kwamba hatuna muongozo na ni jambo ambalo liko katika dini ya Kiislamu na dini zote. Utapata kwamba watu wanatoa sadaka wakienda makanisani. Wanaamini pakubwa kuwa sadaka ile itaenda kujiendeleza katika mambo ambayo watayaona na kuyafurahia. Malengo makubwa ni kwamba mtu apate ujira wa kile alichotoa. Hususan, katika dini ya Kiislamu, hiki ni kitu unachokitoa ambacho kama kilivyoelezewa, kitakuja kukufaa kesho mbele ya Mwenyezi Mungu wakati umeondoka duniani. Kile ukonacho katika ulimwengu huu, utakiacha hapa. Utaenda mbele ya Mwenyezi Mungu ukiwa umeacha kila kitu hapa duniani. Unapoacha kwenye waqf mali yako ama chochote kile ukonacho, ina maana kuwa hata kesho utakapoondoka duniani, kitu kile kitaendelea kukusaidia katika wema wako ambao utapata mbele ya Mwenyezi Mungu. Sio lazima kwa Muislamu ama kwa mtu yeyote ambaye anapaswa atoe hii sadaka ama waqf, bali ni kwa hiari yako. Watu wafahamu vile vile kwamba kitakachopatikana katika waqf hakijatoka katika pesa za Umma. Pesa za Serikali hazitaenda kwenye waqf bali ni zile zitakazotoka kwa watu binafsi ambao watoa kwa hiari yao kwa sababu ya kutarajia malipo ama reward mbele ya Mwenyezi Mungu kesho ahera. Haya yanafanyika kwa ndugu zetu Wakristo na Waislamu. Kwenye huu Mswada wa kiislamu, utaratibu ulioko katika muongozo huu ni kwamba umekuwepo hapo awali lakini haukuwa na natija yeyote katika uislamu. Yameelezewa matatizo kwamba kuna baadhi ya vitu ambavyo vimetolewa kama waqf lakini kwa hivi sasa vinatumiwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}