GET /api/v0.1/hansard/entries/1091521/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1091521,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091521/?format=api",
    "text_counter": 222,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "kwa namna isivyo. Mheshimiwa Mishi ametoa mfano kuwa kuna raslimali ambazo ziko Mombasa zinazotumiwa kwa njia isiyo ya haki. Kwa hivyo, kutokana na hali hii, tume hii ya waqf haiwezikufanya lolote isipokuwa kupitia Bunge hili na kuweza kuweka makaribisho haya kwa usaidizi wa Wabunge ili kuweza kurekebisha na kuendesha utaratibu huu kwa namna yake. Kama nilivyosema, tunao wengi ambao wako tayari kuyafanya haya – kuweka fedha zao na raslimali zao kwenye waqf ili zisaidie jamii. Lakini, inafaa kuwe na muongozo. Hakukuwa na utaratibu au sheria ya kisawasawa. Ndiposa watu wengi walikosa imani ya kufanya jambo kama hili. Ninaamini pakubwa kwamba tutakapopitisha Mswada huu, muongozo kama huu utapatikana na zile hali za jamii kuwa na taharuki ya kwamba pengine wanapopatikana na tatizo la kusoma na kujiendeleza, nafikiri mambo haya yataweza kuepukana na ndugu zetu kama hao katika jamii. Ifahimike kwamba katika maswala haya ya kidini, sote ni ndugu. Utapata kwamba Muislamu anachangia ujenzi wa kanisa na Mkristo vilevile anachangia ujenzi wa msikiti. Kwa hivyo, jambo hili lisilete tafaruku eti kwamba labda pengine kuna muongozo fulani umepangiwa Waislamu kutimiza malengo yao. La. Hii ni kwa sababu wale wanaohusika na utaratibu huu ni wale watakuwa nao. Ninachofahamu ni kwamba hata Waislamu wakiona ndugu zao Wakristo wako na matatizo, wako tayari kuwasaidia lakini ifahamike kwamba ni katika muongozo wa dini ya Kiislamu. Kuna mambo mengine yana muongozo wake. Ifahamike kuwa pesa zozote zitakazokuwa katika waqf, ama raslimali zitakazokuwa pale ni raslimali zitakazochangwa na watu kwa hiari yao. Pesa za Serikali hazitaekezwa pale pengine zisaidie watu waislamu ama wengineo bali ni utaratibu wa kidini ambao umewekwa kwamba unapokuwa na chochote, iwe fedha ama raslimali, unaweka katika waqf ili ikusaidie kesho mbele ya Mwenyezi Mungu. Kile kitu unachoweka ndicho kitakachoangaliwa kisawasawa. waqf ikiangaliwa vyema, itaweza kuwasaidia watu katika jamii. Kwa hivyo, ningependa ndugu zetu Wakristo wafahamu kuwa suala hili halina utata baina ya dini. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}