GET /api/v0.1/hansard/entries/1091715/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1091715,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091715/?format=api",
"text_counter": 122,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia malalamiko ya watu wa Webuye Mashariki katika Kaunti ya Bungoma. Kupokonywa kwa ardhi hii kwa wakaazi hawa wa Webuye ni sawa na yale yalifanyika wakati wa ukoloni. Wananchi walikuwa wanafukuzwa na kufurushwa katika ardhi zao bila ya kufuata sheria. Hata kama msitu huu unajaribu kuweza kulindwa, sio haki wao wasihusishwe. Japo kuwa Serikali inataka kulinda msitu, sio haki wakaazi hawa wasihusishwe katika uamuzi wa kuzuia ama kulinda msitu huu. Sheria iko wazi sasa kwamba jambo lolote ambalo Serikali inataka kufanya mahali popote lazima wakaazi wahusishwe kupitia ile inajulikana kama “ publicparticipation” ama ‘ stakeholder consultation”. Kwa msitu huu, hiyo haikufanyika kwa hivyo hii ni jambo ambalo ni kinyume na sheria. Naomba ile kamati husika isichelewe kutoa uamuzi wa maswala haya. Bi Spika wa Muda, haya ni masuala ambayo yanawahusu makaazi ya wakaazi, mashamba na hata chakula chao. Hii ni kwa sababu wengi ni wakulima na watakosa mahali pa kufanya ukulima wakati msitu huu utakapo chukuliwa. Naunga mkono malalamiko haya ya watu wa Webuye Mashariki. Naomba kamati husika isichelewe kuleta uamuzi kwa Seneti."
}