GET /api/v0.1/hansard/entries/1091717/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1091717,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091717/?format=api",
    "text_counter": 124,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante Sana, Bi Spika wa Muda. Kitu cha kwanza nataka nimpatie kongole sana ndugu yangu mkubwa, Sen. Wetangula, kwa kuleta malalamishi haya katika Bunge hili hususan ikihusikana na watu wake kutoka huko Bungoma. Mwanzo, Waswahili walisema ukiona cha mwenzako cha nyolewa, chako tia maji. Sisi tumekuwa tukinyolewa sana na mambo haya kule pwani. Lakini wakati huu, ninaona kunyoa huku sasa kumefika upande ule wa watu wa Bungoma. Ni jambo la kusikitisha. Jambo la kwanza ni kuona watu ambao wameishi mahali kwa miaka mingi. Wametunza msitu wao. Wameishi na huo msitu. Wanaketi hapo karibu na kushirikiana kuona ya kwamba mazingira yako sawa. Hivi leo, Serikali imeona imefika wakati wa kuweza kutoa notisi la gazeti na kusema hapa tumeweka kama msitu. Ningependa kujiunga na watu wa Bungoma hususan wale wa Webuye ambao hivi sasa wanaonekana wako katika hali ya tahadhari. Hawajui waende mbele ama nyuma. Hawajui hapo ni kwao ama sio kwao na ni mahali wameishi kwa miaka mingi. Bi Spika wa Muda, najiunga nao kusema huu ni ukiukaji wa Katiba. Ikiwa kuna jambo lolote ambalo linahusu na mambo ya wananchi, ni lazima wananchi wenyewe waitwe. Wakae chini, wajadiliane, wakubaliane ili mpango kama huu uchukuliwe na Serikali. Ukifurusha watu 30,000 sio nambari kidogo ambapo kuna akina mama, watoto, mashamba ya watu ambao wenyewe wameketi hapo miaka mingi. Wamejenga makanisa, shule, nyumba na kuweka maisha yao hapo. Kunao hata makaburi na kanisa. Hivi leo"
}