GET /api/v0.1/hansard/entries/1091799/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1091799,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1091799/?format=api",
    "text_counter": 206,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii kumpongeza Sen. Iman kwa kuzungumzia mambo ya kujitoa uhai katika Taarifa yake. Hili ni jambo ambalo linatia watu wengi hofu kwa sababu limekuwa kawaida mtu kujiua ama kua wendani wake kisha anajiua bila sababu yoyote maalum. Inafaa tuangazie uwezo wa dini zetu. Wahubiri watasaidia swala hili. Swala la kujitoa uhai linalingana na imani yako katika dini. Ikiwa imani yako ni nyepesi, utakuwa hatarini zaidi kujitoa uhai kuliko yule ambaye imani yake ni dhabiti. Ninafikiri Sen. Wambua ambaye ni mhubiri anaweza kushuhudia swala hili. Lazima tulete taasisi za ushauri nasaha ili wale ambao wana matatizo kama haya waweze kupata fursa ya kushauriwa. Aitha iwe katika makanisa au miskiti. Huduma kama hizo zipatikane kwa urahisi ili yeyote ambaye ana matatizo kama haya asaidike. Bi. Spika wa Muda, inafaa pia tuangalie maadili yetu. Hivi sasa, wengi wetu tumeweka maisha ya kifahari mbele. Wakati matatizo yanatokea kidogo, unapata kuwa wale wendani wako uliolukuwa nao katika mfumo wa maisha wamekuwacha. Hiyo iakufanya usiwe na imani kuwa maisha yako inaweza kuwa bora kuliko wale. Kwa hivyo, inafa pia tuanagalie maadili zaidi kwa sababu tukichunga maadili, itapunguza nafasi ya mtu kujitoa uhai bila sababu yoyote. Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii."
}