GET /api/v0.1/hansard/entries/1092690/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1092690,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1092690/?format=api",
    "text_counter": 66,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ninasimama kwa Hoja ya Nidhamu. Kulingana na sheria zetu, ni haki kuongea juu ya mtu ambaye hayumo humu Bungeni, ama katika nafasi ya kujitetea, kisha tena uongee kwa njia isiyo na heshima? Lazima tuwaheshimu viongozi wetu. Sisi sote ni Waafrika na tunajua heshima kwa mtu mzima aliyekupita kwa umri ni jambo la muhimu. Hapa yeye haongei juu ya mtu asiye muhimu. Huyo ni muhimu tena mkubwa wake kwa umri na hata anaweza kuwa baba yake. Kwa hivyo, itakuwa ni matusi Sen. Murkomen kutumia lugha isiyofaa kwa kiongozi wa taifa hili ambaye ameleta amani humu nchini. Ni makosa sana. Je, ni haki kutaja mtu asiyeweza kujitetea ndani ya hili Bunge; hususan kutaja kiongozi wa Chama cha ODM mimi nikiwa mwanachama wake?"
}