GET /api/v0.1/hansard/entries/1094059/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1094059,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1094059/?format=api",
    "text_counter": 188,
    "type": "speech",
    "speaker_name": ".Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "zinapata crack, watu wanakuwa wagonjwa, viziwi na hata wengine wanapata ugonjwa wa saratani. Mawe ambayo yanatumika kujenga katika maeneo ya pwani yanatoka upande wa Kilifi ilhali watu wa Kilifi wanabaki maskini. Kila upande wa bahari kumetobolewa mashimo na watu ambao wako na pesa na wazungu ambao wamenunua vifaa. Hao watu wanatengeneza pesa na kuacha watu wa hayo maeneo katika hali ya umaskini. Huu Mswada utawezesha watu kufaidika kutokana na madini ambayo yanapatikana katika maeneo yao. Chumvi ambayo inatumika Kenya nzima inatoka Magarini, Kilifi, ilhali wafanyikazi katika hizo viwanda, ambao ni wenyeji wa Magarini, wanapata taabu. Wengi wao wanakuwa wagonjwa kwa sababu hawana vifaa vinavyohitajika. Mazingira yao ni mbovu ilhali watu wote nchini Kenya wanakula chumvi inayotoka Kaunti ya Kilifi. Huu Mswada utasaidia maneno kama hayo. Mchanga inatoka Mjanaheri ambayo ni eneo ya Magarini, Kaunti ya Kilifi. Hiyo mchanga yote inatoka kwetu ilhali wakaazi hawafaidiki na rasilimali yao. Hiyo ndiyo ninasema ya kwamba hiyo sio sawa. Mswada huu unataka hao wakaazi wafaidike na rasilimali zao. Tuko pia na Limestone. Wananchi wa hayo maeneo wanaweza kufaidika kwa sababu tuko na viwanda viwili vya saruji katika Kaunti ya Kilifi. Kiwanda cha Mombasa"
}