GET /api/v0.1/hansard/entries/1094061/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1094061,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1094061/?format=api",
    "text_counter": 190,
    "type": "speech",
    "speaker_name": ".Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "peke yake ndicho kina zingatia mazingira na ndiyo inasaidia watu wa hayo maeneo. Tunataka hizo viwanda zote ziwe na corporate social responsibility na sio Mombasa Cement peke yake. Ukienda Kaunti ya Kwale, tuko na titanium ambayo ni mchanga wa thamani sana. Iko kama almasi. Huo mchanga pia unapatikana upande wa Mrima ambapo ni mlima kubwa. Mchanga kutoka Mrima huwa unatumika kutengeneza ndege ambazo zina safirisha abiria. Huu Mswada una umuhimu zaidi. Ninampa dadangu, Sen. (Dr.) Zani, ambaye anatoka maeneo ya Kaunti ya Kwale, kongole kwa sababu amesaidia huu Mswada utasaidia watu ambao wanaishi katika yale maeneo. Ni laziima ugavi kama huu uzingatiwe sawasawa na kusiwe na ufisadi. Tuko pia na mazeras ambayo watu wengine wanaita galana stones . Watu wengine wanazitumia kutengeneza tiles . Kaunti ya Kwale iko na madini kama hayo na ndio maana wanafaa kupewa nafasi ili wafaidike. Sisi watu wa Kaunti ya Kilifi hatuwezi kusema ya kwamba tunafaidika kutokana na rasilimali ambayo tuko nayo kwa sababu watu wetu wanateseka ilhali tuko na rasilimali. Ni lazima serikali izingatie na kuona ya kwamba watu wa Kaunti ya Kilifi wamefaidika kutokana na rasilimali yao. Shida kubwa huwa ni wakurungenzi wa kampuni wanaonyanyasa wananchi wa viwango vya chini na hiyo ni mbaya. Watu hupata ugonjwa kama saratani, wengine wanakuwa viziwi na hata vipofu. Huu Mswada utaweza kuokoa maisha ya wakenya ambao wanaishi katika maeneo ambayo yana madini kama kaunti za Kilifi, Kwale na hata Taita Taveta. Watu wa Taita Taveta wanateseka sana ilhali wako na mawe ya thamani sana."
}