GET /api/v0.1/hansard/entries/1094453/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1094453,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1094453/?format=api",
    "text_counter": 335,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
    "speaker": {
        "id": 13274,
        "legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
        "slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
    },
    "content": " Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nichangie Mswada huu ulio muhimu sana. Ninampongeza Mhe. Rehema Jaldesa kwa kulifikiria hili jambo na kulileta hapa ili tulijadili. Ni kweli, kumekuwa na ukame. Hata tunahofia kwamba tutaanza kupoteza watu wetu na mifugo kwa ajili ya njaa. Katika kaunti yangu ya Taita Taveta pia kuna ukame sampuli mbili. Sampuli ya kwanza inasabibishwa na ukosefu wa mvua na maji. Sampuli ya pili inasababishwa na wanyamapori. Hii ni kwa sababu tumezungukwa na mbuga ya wanyama pori. Katika zile sehemu chache ambako mvua imenyesha na watu wamepanda mimea, wanyamapori wanavamia na kula kila kitu na wananchi wanabaki bila. Swala hilo linatupa hofu kubwa kwa sababu ikiendelea hivyo, basi wanyama pori watatoka porini na wakikuta kumekauka namna hiyo watawavamia binadamu na watu watapoteza maisha. Tayari tushaona ndovu wakitoka na kuelekea mahali wananchi wako. Wameanza tabia ya kupasua matangi ya maji. Hii ni kwa sababu ya ukame. Wakikosa chakula na maji kwenye mbuga wanavamia makazi ya binadamu na kupasua matangi ili wapate maji ya kunywa. Itakuwa vyema nikiwaunga mkono wenzangu waliotangulia kuongea ili tulitaje hili kama janga la kitaifa ili liweze kuchukuliwa kwa uzito unaostahili na liweze kushughulikiwa ili tusiendelee kupoteza maisha. Tayari tumeshapoteza wapendwa wetu wengi kupitia hili janga la Korona na hatutaki kuwapoteza watu zaidi kwa sababu ya mambo ambayo tunaweza kuyafanyia kazi. Asante."
}