GET /api/v0.1/hansard/entries/1094927/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1094927,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1094927/?format=api",
"text_counter": 43,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Mhe. Spika kwa kunipatia hii fursa na mimi niweze kuchangia. Nataka kusema utalii umekuwa nguzo ya uchumi wa Kenya, haswa kule Pwani. Tumewaona mabwana wale ambao huwaongoza watalii na kuwaonyesha maegesho na sehemu tofauti tofauti. Wamekuwa wakifanya kazi nzuri ila hawajatambulika kwa muda mrefu sasa. Nimefurahi sana kwa ajili ya ombi hili ambalo limeletwa hapa. Naomba sana lipate kibali hapa hasa katika Kamati husika ambayo itaenda kufanya kazi. Hawa wanaowaongoza watalii sharti wapate haki ili tuweze kuboresha utalii hapa Kenya kama vile ilivyokuwa mwanzoni. Asante Mhe. Spika."
}