GET /api/v0.1/hansard/entries/1095117/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1095117,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1095117/?format=api",
    "text_counter": 233,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": " Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Hata mimi nasimama kuunga mkono Mswada huu ambao unataka kuleta marekebisho kwa sheria inayozungumzia bima ya afya ya kitaifa ndiyo Wakenya wote waweze kupata afya bora. Afya imekuwa changamoto sana kwa Wakenya wetu haswa tukizingatia kumekuwa na matatizo na maradhi sugu kama saratani, kisukari na COVID ambayo tunaita korona. Tunajua Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye ni Raisi wetu katika liwaza yake ama zile Shabaha zake Nne, moja ni kuhakikisha kwamba Wakenya wote wataweza kupata afya sawia hata matajiri. Tukiangalia nchi zilizostawi ulimwenguni, tunaona ya kwamba suala la afya limepewa kipau mbele. Ambapo yule maskini na tajiri wanaweza wote kwenda katika zahanati ambayo imestawi vilivyo kwa upande wa madawa na vifaa vya kiafya na kupata matibabu kwa njia ya usawa. Mswada huu pia unazungumzia bodi ambayo itasimamia bima hii ya kitaifa ya afya. Watahakikisha kwamba wamekaa na washikadau na wahusika wote katika mazungumzo ili kuhakikisha kwamba afya itapatikana kwa Wakenya wote. Vile vile tunauunga mkono Mswada huu lakini pia kuna sehemu ambazo tunataka tulete marekebisho. Kama sehemu inayosema The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}