GET /api/v0.1/hansard/entries/1095118/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1095118,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1095118/?format=api",
    "text_counter": 234,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "kwamba lazima yule mwajiri na mwajiriwa waweze kulipa kiwango sawia kilicho sawa. Lakini lazima tuzingatie ya kwamba kuna wajiriwa wengi Wakenya wetu ambao ni maskini na mapato yao ni machache. Utapata ya kwamba mtu anafanya kazi katika kampuni inayopata mapato makubwa, imestawi na ambayo inaweza kutoa mchango mkubwa katika kufidia bima hii. Ni bora iwapo kampuni kama ile ambayo ina uwezo zaidi na mapato yake yako juu, mchango wao uwe mkubwa zaidi ya yule aliyeajiriwa. Hii ni kwa sababu walioajiriwa wanapata mapato ya chini sana na hawawezi kupata sawia na ule mwajiri ambaye anafaidika zaidi kutokana na biashara ya ile kampuni. Vile vile pia ibara moja inazungumzia kwamba ukifika miaka 18, iwapo haujaingizwa katika bima hii ya kitaifa ya afya, itakulazimu ulipe ule mchango unaohitajika. Na wenzangu wamesema kwamba Kshs.500 ni pesa nyingi. Nataka niwaunge mkono haswa tukizingatia hivi sasa tuko na changamoto za kiuchumi ambazo zimesababishwa na maradhi hatari ya korona. Wakenya wengi hivi sasa hawako katika ajira ama katika biashara zao. Hivyo basi, itakuwa ngumu iwapo pengine ni kijana ambaye hana baba wala mama ni yatima, na anaambiwa lazima akifika miaka 18 aweze kulipa mchango kama huu. Lazima tutafute mbinu za kuonyesha kwamba yale makundi ambayo yako katika hali ngumu, yale kwa Kingereza tunaita vulnerable groups, yatazingatiwa kwa njia gani. Ili waweze kutoa mchango huu wa kufidia wa bima hii ya kitaifa ya afya ndio watu wote wapate afya. Vile vile katika kuorodhesha zile zahanati ama hospitali ambazo zitatibu Wakenya kwa kupitia bima hii ya kifaita ya afya, lazima ziorodheshwe zahanati ambazo zimestawi, zinamiondo misingi ya kiafya. Kwa mfano, zahanati ambayo inaweza kufanya operesheni ya majongwa magumu kama ya moyo. Pia lazima hizi zahanati ziwe na vifaa vya kisasa, madawa na Wakenya wanaweza kufikia. Kwa hivi sasa, Wakenya wengi ambao wako na hii bima ya afya ya kitaifa wana kadi. Unapata mpaka mtu atembee kilomita mingi ama mwendo wa siku moja ama mbili ndiyo aweze kufikia zahanati anayoweza kutoa ile kadi na kupata matibabu. Kwa hivyo, lazima tuaangalie wakati tunafanya mpango kama huu na kuleta Mswada huu wa marekebisho orodha ya zahanati ambazo tutaweka ziwe zile Wakenya wataweza kufikia. Na wakati Wakenya wanafika katika zahanati kama zile, isiwe kama haya yanatokea sasa. Unafika pale na kuambiwa kwanza lazima simu ipigwe na pengine mtu amepata dharura kama ya ajali ama maradhi ya ghafla. Anaambiwa lazima wapigiwe simu ndiyo wapate ruhusa kwamba wanaweza kumchukua kupitia kadi ile ya hazina ya bima ya kitaifa ya afya. Lazima mikakati kama hiyo iweze kuwekwa hivi sasa, kwa sababu tuko katika mambo ya digitali ama teknolojia ya kisasa. Lazima kuwe na njia ambazo hazitakuwa za kadi ama stampu ya kuorodesha ambazo zitamuwezesha yule Mkenya aliye pale mashinani ambaye pengine atakuwa hawezi kupitia teknolojia ya kisasa au hawezi kupitia mambo ya simu kwa njia ambazo zitakuwa mwafaka na zile hali za mazingira yetu sisi kama Wakenya. Vilevile pia nataka niseme kwamba naunga mkono kwa sababu Mswada huu unasema utaboresha miundo msingi ya zile zahanati. Hivyo basi, ni vizuri kwamba kaunti zetu ambazo hivi sasa afya imegatuliwa, ziweze kuwa sawia na Mswada huu na ziweze kuhakikisha kwamba zile zahanati ambazo wamezijenga, wamezijenga hali ya kwamba ziko sawia na miundo msingi kupambana na maradhi magumu na sugu. Hivi sasa Wakenya wengi wanakufa kwa sababu ya kukosa oxygen na hivi sasa ni masikitiko. Tunasikitika na tunasema pole. Tumempoteza dada yetu mpendwa aliyekuwa Mbunge Mwakilishi wa Kina Mama katika Kaunti ya Kwale, Mhe. Zainab Chidzuga. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake pema. Ni kwa sababu tumekuwa na changamoto ya oxygen . Tuko na zahanati zingine kule mashinani lakini unapata mtu anapopatwa na tatizo hili la COVID-19, anaambiwa lazima aende katika hospitali kubwa. Kama pengine ni kule kwetu Mombasa unaambiwa ni Coast General, Mombasa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}