GET /api/v0.1/hansard/entries/1095119/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1095119,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1095119/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Hospital au Aga Khan na hizo hospital zingine ni za watu binafsi ambazo pia malipo yao yako juu sana. Hata ukiwa na kadi, haiwezi kukusaidia kulipa malipo kama hayo. Kwa hivyo, ningesema kwamba mambo haya yote lazima yazingatiwe sana. Vilevile katika Mswada huu tunajua pia kuna ufisadi ambao umekuwa ukitendeka katika Hazina hii ya Kitaifa ya Bima ya Afya. Lazima kuwe na mikakati ya kuangalia je ufisadi kama huu ambao watu wametumia njia fulani kuiba fedha kama hizi ambazo zingemsaidia Mkenya katika mambo ya afya iangaliwe kwamba mashimo kama yale yatazibwa na itaweza kuangalia kwamba hakutakuwa kamwe na mambo ya ufisadi ambayo hivi sasa sisi kama Wakenya na kama viongozi hapa Bungeni, tunajua yametokea katika hazina hii. Ningeomba kusema kwamba zile penalty ambazo tunaambiwa watu ambao hawatakuwa wamelipa watatozwa lazima pia kuwe na vifungu vya kuonyesha zitatumika kwa njia gani kwa sababu pengine mtu amekuwa mgonjwa au ana changamoto fulani hakuweza kulipa na anaambiwa kwamba atalipa ile penalty na wakati huu mgumu wa korona itakuwa ni matatizo. Kwa hivyo, lazima tuwe na njia mwafaka za kuonyesha penalty hizi zitaweza kuwekwa kwa wale ambao wanaonekana haswa hawa ni kwa makusudi wamekataa kulipa mchango huu wa Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya lakini si kwa wale ambao watakuwa wana matatizo ambayo yanaeleweka. Kama vile dadangu alivyosema, kuna wale walemavu, watoto na watu wazima. Hawa ni watu ambao lazima tuwasaidie kupata afya bure katika taifa letu kwa sababu hata nao asilimia yao iko hapa kwetu Kenya na wanahitaji na wao pia wana changamoto nyingi za kiafya. Hivyo basi, lazima tuwape kipau mbele katika afya kwa wote. Hao ndio watu ambao tutawazingatia zaidi…"
}