GET /api/v0.1/hansard/entries/1096613/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1096613,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1096613/?format=api",
    "text_counter": 126,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika. Naomba usaidizi kutoka kwako na pia utoe amri. Tarehe 16 Juni 2021, niliinuka katika Jumba hili baada yako kuweka sahihi na kupeana idhini ya kutuwezesha kuulizia hatma ya wafanyikazi wa Shirika la Bandari ya Kenya yaani Kenya Ports Authority (KPA). Mambo yalikuwa ni matatu. Kwanza, ule mkataba uliokubaliwa wa nyongeza ya mishahara. Pili, kando na yale ambayo washakubaliana, ni njia gani ambayo wataanza kuzungumzia habari ya makubaliano mapya? Tatu, wale wafanyikazi 247 waliofutwa wanaofaa kuregeshwa. Nilielekeza Swali hilo kwa Kamati inayohusika na mambo ya usafiri lakini chini ya amri yako, ukasema iende kwa Kamati ya Leba. Walidokeza kuwa kwa muda wa wiki moja, wataweza kutupa jawabu. Leo hii, tumemaliza miezi miwili ya Juni na Julai. Tuko mwezi wa Agosti. Nilipokuwa naingia hapa, niliambiwa kuwa kuna jawabu ambalo limetolewa na Waziri Ukur Yatani. Ukiangalia hali ilivyo, tulielezewa kuwa Julai mwaka huu, uchumi wa nchi hii ulipanda kwa asilimia 6.44. Haijawahi kufika hivyo katika miezi kumi na saba. Juni mwaka huu, ilipanda kwa asilimia 5.87. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}